RAILA AWASILISHA RASMI AZMA YA AUC

Kenya imewasilisha rasmi azam ya kinara wa ODM Raila Odinga kuwania wadhifa wa uwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AUC kwa Mkuu wa umoja wa Afrika kanda ya mashariki ambaye pia ni Balozi wa Mauritius Dharmraj Busgeeth.
Katibu katika wizara ya masuala ya kigeni Korir Sing’oei akiwa amendamana na mwandani wa Odinga Makau Mutua na balozi wa Kenya nchini Ethiopia George Orina, amesema wamewasilisha stakabadhi hitajika kwa mujibu wa kanuni za tume hiyo.
Hatua hiyo inaweka wazi kujitolea kwa serikali katika kuongoza azma ya Odinga baada ya shauku kuibuka kutokana na maandamano ya kupinga uongozi mbaya serikalini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa