#Local News

WACHA WATOTO NAIROBI WALE, MAHAKAMA

Jaji wa mahakama kuu Chacha Mwita ametupilia mbali kesi ya kupinga mpango wa lishe shuleni maarufu kama Dishi na Kaunti chini ya serikali ya kaunti ya Nairobi, akisema kusitisha mpango huo ni ishara ya kutojali maslahi ya wanafunzi.

Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa na kikundi cha Tunza Mtoto Coalition Kenya kupinga mpango huo kikisema ni haramu kwani elimu ni jukumu la serikali ya kitaifa na wala si ya kaunti.

Hata hivyo, serikali ya kaunti kupitia wakili wake Duncan Okatch ilijitetea ikisema taratibu zote zilifuatwa kabla ya kuanzishwa kwa mpango huo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WACHA WATOTO NAIROBI WALE, MAHAKAMA

ERIC OMONDI AKAMATWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *