#Local News

HATUA ZA KITAALAMU ZA KUKABILI MABADILIKO YA HALI HEWA MASHINANI

Mpango wa ufadhili wa kijani wa Kenya uko katika hatua mahususi kwa wenyeji kuthibitisha mikakati yao katika kutekeleza miradi ya kuwaendeleza ndani ya maeneo yao kutokana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi.

Ofisi tanzu ya Hazina inayoshughulikia mpango wa Ufadhili wa Hali ya Hewa ya Ndani imethibitisha kushuhudia pengo la maarifa ya mabadiliko ya tabianchi katika hatua mbalimbali za mpango huo katika kaunti zote 47.

Kulingana na wataalam wa masuala ya hali ya hewa nchini Kenya, vitengo vya utekelezaji vya kaunti vinahitaji kuongozwa kupitia michakato mara nyingi zaidi na vile vile wenyeji ambao wako mstari wa mbele katika kutekeleza miradi ya hali ya hewa, katika juhudi za kukabili mabadiliko ya tabianchi.

Imetayarishwa na Janice Marete

HATUA ZA KITAALAMU ZA KUKABILI MABADILIKO YA HALI HEWA MASHINANI

ROMANIA YAFIKA ROBO FAINALI

HATUA ZA KITAALAMU ZA KUKABILI MABADILIKO YA HALI HEWA MASHINANI

EMERGING STARS WAZIDI KUTAMBA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *