NYOTA YA MADINA YAREJESHWA

Mchezaji wa mpira wa vikapu Madina Okot hatimaye anaweza kupumua baada ya kupata visa yake ya kusafiri kuelekea Marekani baada yapita vigezo vya ukiritimba.
Baada ya kusubiri kwa miaka mwiwili, Okot anatazamiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Jimbo la Mississippi, ambapo ataboresha ujuzi wake na kupata uzoefu muhimu katika kiwango cha chuo.
Okot alipewa visa siku ya Jumanne, na kumtengenezea njia ya kuelekea Marekani.
Msichana hiyo alikabiliwa na vikwazo katika majaribio yake ya awali, baada ya kuomba visa mara tatu bila mafanikio.
Hata hivyo aliendelea kuwa mvumilivu, akidhamiria kutimiza ndoto yake ya kucheza kitaaluma.
Shukrani kwa NBA Kenya, sasa yuko tayari kwa safari ya kusisimua.
Imetayarishwa na Nelson Andati