TETESI ZA UHAMISHO- SOKA ULAYA MSIMU HUU WA JOTO

Kwenye tetesi za uhamisho ulaya msimu huu wa joto ni kwamba, kiungo wa kati wa uingereza na Lille Angel Gomes,24, anatazamiwa kujiunga na Newcastle united ila Liverpool, Tottenham na Borussia Dortmund pia wanafanya juhudi kuhakikisha wanamnyakua mchezaji huyo.
Hii ina maana kuwa gomes, atakuwa na kibarua kikubwa cha kuchagua timu bora inayowiana na mbinu yake ya uchezaji miongoni mwa hizo timu tatu.
Na klabu ya West Ham wamepokea ofa kutoka kwa Galatasaray kwa ajili ya beki wa Italia Emerson Palmieri, 30.
Huku Manchester City, Chelsea na Liverpool wakimwinda kiungo wa kati wa Sunderland muingereza Chris Rigg, 17.
Imetayarishwa na Osoro Kennedy