#Football #Sports

GREGG APIGWA KALAMU

Kocha wa timu ya taifa ya Marekani Gregg Berhalter amepigwa kalamu kufuatia timu yake kutolewa katika raundi ya kwanza kwenye michuano ya Copa America.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50, ambaye alirejeshwa tu kuifundisha timu hiyo mwaka jana, na alishindwa na Panama na Uruguay baada ya kuishinda Bolivia kwenye mechi ya kwanza.

Hii ilikuwa mara ya kwanza katika historia kwa taifa mwenyeji wa Copa America kuondolewa katika raundi ya kwanza na ikaongeza shinikizo la kufutwa kwake.

Hatua hii inajiri miaka miwili tu kabla ya Amerika kuandaa kwa kwa pamoja Kombe la Dunia na Canada na Mexico mnamo 2026.

Imetayarishwa na Nelson Andati

GREGG APIGWA KALAMU

COLOMBIA WAWATEKA URUGUAY

GREGG APIGWA KALAMU

SINA WASHAURI; DUALE AIAMBIA PSC

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *