KAUNTI ZAONGEZEWA MGAO
Hatimaye vuta nikuvute kuhusu mgao wa serikali za kaunti imepata suluhu baada ya kamati ya Pamoja ya wabunge na maseneta kuafikiana shilingi bilioni 415 kwa serikali hizo kwenye mwaka wa kifedha wa 2025-26.
Mgao huo ni nyongeza ya shilingi bilioni 27.6, kutoka bilioni 387.4 kwenye mwaka huu unaokamilika wa kifedha.
Aidha, hii ni nyongeza ya shilingi bilioni 10 kutoka bilioni 405 zilizokuwa zimependekezwa na wizara ya fedha.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































