MADEREVA WA TEKSI WAANDAMANA MOMBASA KULALAMIKIA KIFO CHA MMOJA WAO

Shughuli za uchukuzi zimetatizika mjini Mombasa kufuatia maandamano ya Madereva wa teksi za mtandaoni mjini wakishinikikza haki itendeke kwa wenzao ambao wamethulumiwa na wengine kuuawa.
Wametoa mfano wa kifo cha mwenzao Victoria Mumbua ambaye aliuawa na gari lake kuibiwa.
Madereva hao wameeleza kuwa wanahofia Maisha yao kwa kuwa kulingana nao maafisa wa usalama hawajakuwa wakiwalinda ipasavyo,sasa wanaitaka serikali ya kitaifa kuingilia kati na kuwahakikishia usalama wao wanapokuwa kazini.
Imetayarishwa na Janice Marete