#Local News

POLISI WAMHUSISHA GACHAGUA NA MAANDAMANO

Polisi wamewahoji wasaidizi watatu wakuu wa naibu Rais Rigathi Gachagua na wabunge wawili kutoka kaunti ya Nairobi kuhusiana ufadhili wa maandamano ya kupinga mzigo wa ushuru na uongozi mbaya serikalini.

Kwenye uchunguzi huo, polisi wamezuru afisi za wasaidizi hao mtaani Karen ambako wamechukua taarifa za maafisa hao, huku makachero wa DCI wakiendelea kuchunguza visa vya uharibu na uporaji wa mali jijini Nairobi na maeneo ya kati ya nchi.

Aidha, polisi wamesema wanatarajia kuchukua taarifa kutoka kwa viongozi kadhaa wa kisiasa akiwemo gavana wa zamani.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *