#Local News

KISA CHA PILI CHA MPOX CHAGUNDULIWA KENYA

Kisa cha pili cha ugonjwa wa Mpox kimegunduliwa humu nchini, Waziri wa afya Deborah Mulongo akisema kisa hicho kimegunduliwa baada ya sampuli kutoka kwa dereva wa trela katika mpaka wa Kenya na Uganda mjini Malaba kaunti ya Busia kufanyiwa vipimo.

Amesema mgonjwa huyo amewekwa karantini katika kituo kimoja cha afya kaunti ya Busia ambako anatibiwa.

Aidha, Mulongo amesema kuwa vipimo vimeimarishwa katika eneo hilo na kaunti nyingine kote nchini, akisema hadi sasa sampuli kutoka kwa watu 42 zimechunguzwa, 2 zikirejesha matokeo ya kuwepo kwa ugonjwa huo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *