SIASA MBAYA MAISHA MBAYA

Zaidi ya shilingi bilioni 608 hupotea kila mwaka humu nchini kupitia uifisadi, mwingiliano wa kisiasa ukitajwa kuwa kikwazo kikubwa katika kutoa haki kwenye kesi mbali mbali za ufisadi.
Haya ni kulingana na ripoti ya shirika la Transparency International, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Shilla Masinde akisema kesi nyingi zimekosa kuendelea kutokana na mwingiliano wa wanasiasa.
Nayo tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC imesema licha ya kuwepo kwa sheria za kutosha za kukabili ufisadi, zimekuwa zikipuziliwa mbali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa