GACHAGUA: MAHAKAMA YAMPA PIGO JINGINE
Naibu Rais Rigathi Gachagua sasa atalazimika kufika mbele ya bunge la seneti wakati wa kusikilizwa kwa hoja ya kutimuliwa kwake kutoka afisini baada ya mahakama kuu kudinda kutoa amri ya kusitisha vikao hivyo.
Jaji wa mahakama hiyo Chacha Mwita, ametoa uamuzi huo licha ya Gachagua kupitia kwa mawakili wake kutaka mahakama isitishe vikao hivyo ambavyo vinatarajiwa kuanza hapo kesho.
Kwenye kesi hiyo, mawakili wa Gachagua wanashikilia kwamba hoja ya kutimuliwa kwa mteja wao imechochewa kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































