#uncategorized

UPINZANI WAANZA ZIARA YA SIKU 5 MAGHARIBI, RIFT VALLEY

Viongozi wanaoegemea mrengo wa upinzani wameendeleza juhudu za kujitafutia uungwanji mkono kwenye uchaguzi mkuu ujao, wakiratibu misururu ya mikutano ya kisiasa na wakazi wa maeneo ya Magharibi na bonde la ufa.

Mikutano hiyo ya wiki nzima inaanza hii leo katika kaunti 10, ikiongozwa na kinara wa DCP Rigathi Gachagua, Kalonzo Musyoka wa Wiper, Eugene Wamalwa wa DAP-K, na Martha Karua wa PLP.

Wengine ni Justin Muturi na waziri wa zamani Fred Matiang’i, wakiapa kuhakikisha Rais William Ruto hachaguliwi kwa muhula wa pili.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *