MWANAUME AKAMATWA KWA KUMUUA BINAMU YAKE MIGORI

Polisi wamemkamata mwanamume wa miaka 27 kwa madai ya kumchoma kisu na kumuua binamu yake wa miaka 21 katika Kaunti ya Migori.
Kulingana na Naibu Chifu William Jabed, ugomvi kati ya wawili hao umesababisha mshukiwa, Fred Ngere, kurejea nyumbani kuchukua kisu kabla ya kumshambulia Charles Otieno, aliyefariki alipofikishwa hospitalini.
Mwili wake umehamishiwa Hospitali ya Migori Level Four kwa uchunguzi wa maiti.
Imetayarishwa na Janice Marete