#Local News

“IMFIKIE INJENDI!”- WAANDAMANAJI MALAVA

Kundi la vijana waliokuwa wakiandanmana wamevamia mkutano wa mwakilishi wa kike kaunti ya Kakamega Elsie Muhanda uliokuwa ukiandaliwa katika eneo bunge la malava wakimsaka mbunge wa eneo hilo Malulu Injendi ambaye alipiga kura ya ndiyo kuhusu mswada wa fedha wiki jana.

Vijana hao wamechukua usimamizi wa hafla hiyo na kuamuru kwamba mbunge huyo asiondoke na walipobaini kwamba hakuwepo, wamemtaka Muhanda amweleze mbunge huyo ajiuzulu kutokana na uamuzi wake wa kuunga mkono mswada huo

Vijana hao wamekuwa wakiandamana kwa amani mjini Malava kabla ya kuvamia mkutano huo, siku moja baada ya mbunge huyo kufurushwa kutoka hafla moja eneo la Musingu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

“IMFIKIE INJENDI!”- WAANDAMANAJI MALAVA

KENYA MBIONI KUMALIZA EUROBOND

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *