MAELEKEZO YATATOLEWA KATIKA KESI YA KUPINGA MSWADA WA FEDHA ULIOONDOLEWA

Mahakama ya Juu leo hii itatoa mwelekeo katika kesi ambapo mawakili na Wanasheria wa eneo la Mlima Kenya waliwasilisha kesi kupinga kutekelezwa kwa mswada wa fedha 2024-2025.
Mnamo Juni, kundi la mawakili na Wanasheria wa Mlima Kenya walielekea mahakamani wakitaka amri ya kumzuia Rais William Ruto asiidhinishe Mswada wa Fedha na Ugawaji wa Fedha, 2024 uliokumbwa na utata, ikisubiri kuamuliwa kwa ombi hilo.
Ombi lililowasilishwa na mawakili wakiwemo Ndegwa Njiru, Lempaa Suyinka, Fanya Mambo Kinuthia, Peter Koira, Ishmael Muriithi, Jackline Mwangi, Charles Mabiru, pamoja na Chama cha Wanasheria wa Mlima Kenya, lilionyesha kuwa maombi yao yalichochewa na hatua ya wabunge kupitisha mswada wa ushuru wenye utata licha ya upinzani kutoka kwa Wakenya wengi.
Imetayarishwa na Janice Marete