MSHUKIWA WA MAUAJI YA KWARE AKIRI KUWAUA WANAWAKE 42 – DCI YASEMA
Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) imefichua kuwa mshukiwa mkuu wa miili iliyogunduliwa Kware, mtaa wa mabanda wa Mukuru, Nairobi, aliwaua wanawake 42.
Kwa mujibu wamkurugenzi mkuu wa DCI Mohamed Amin mshukiwa kwa jina Collins Jomaisi Khalisia baada ya kuhojiwa, amefichua kuwa aliwaua wanawake hao 42 kati ya mwaka 2022 na tarehe 11 mwezi julai alipomuua mwathiriwa wake wa mwisho na kutupa miili yao katika eneo la kutupia taka ndani ya miaka miwili.
Mshukiwa amedai kuwa mwathiriwa wa kwanza alikuwa mkewe ambaye alimnyonga hadi kufa na kumkatakata na kumtupa kwenye eneo hilo.
Imetyarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































