#uncategorized

TUME YA HUDUMA ZA UMMA PSC YATANGAZA NAFASI ZA AJIRA

Tume ya huduma za umma PSE imetangaza nafasi 532 za ajira kwenye idara mbali mbali za serikali.

Katika notisi iliyochapishwa kupitia gazeti la rasmi la serikali PSE imetangaza nafasi moja ya mkuu wa mawasiliano katika wizara ya habarimawasiliano na teknolojia.

Katika idara ya huduma za afya PSE inalenga kuwaajiri maafisa 23 huku watu 177 wakiajiriwa katika wizara ya usalama na maswala ya ndani ya nchi.

Wengine 106 wataajiriwa katika wizara ya ulinzi aidha inalenga kujaza nafasi 19 kwenye idara ya vyama vya ushirika ( cooperatives).

Nayo idara ya mazingira na tabia nchi pse imetenga nafasi 69 huku wizara ya leba ikitengtewa nafasi  144.

Pse inalenga kuwaajiri maafisa wawili katika wizara ya afrika mashariki na maeneo kame , nafasi ya naibu m kuu wa chuo kikuu cha Tuk pia imetangazwa na pse.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *