BENJAMIN SESKO AVUTIWA NA ASENALI
RB Leipzig wanataka dili la thamani kati ya £68.4m [€80m] na £85.5m [€100m] kwa ajili ya Benjamin Sesko anayelengwa na Arsenal.
Arsenal walifanya mazungumzo ya awali na Leipzig kuhusu mshambuliaji huyo msimu huu wa joto, lakini hadi sasa hakujakuwa na ofa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo ya Ligi ya Premia.
RB Leipzig sasa wako tayari kumwacha aondoke baada ya kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
Sesko alifunga mabao 21 na alitoa pasi za mabao sita katika michuano yote msimu uliopita, ikijumuisha manne kwenye Ligi ya MabingwaIsak ni ngumu sana – Newcastle hawataki kuuzwa na thamani yake ni kubwa – hivyo hakuna uwezekano mkubwa kutokea katika hatua hii.
Arsenal wamefanya mazungumzo ya awali na RB Leipzig kuhusu Sesko ili kuchunguza masharti ya mkataba huo.
Arsenal pia bado wanavutiwa na mastaa kama Rodrygo wa Real Madrid katika nafasi ya winga.
Klabu hiyo ina uhakika wa kukamilisha usajili wa kiungo wa Real Sociedad Martin Zubimendi.
Imetayrishwa na Nelson Andati
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































