UPATANISHI WA LAZIMA NI MUHIMU: JAJI REUBEN NYAKUNDI

Jaji wa mahakama kuu ya Eldoret Reuben Nyakundi anataka upatanishi wa lazima yaani MADATORY MEDIATION kuhidhinishwa katika kutatua baadhi ya kesi zinzowasilishwa mahakamani.
Kwa mujibu wa Nyakundi hatua hiyo itasaidi kupunguza mrundiko wa kesi makakamani na kuharakisha kupata haki kwa wahusika.
Nyakundi vile vile ameongeza kuwa mazungumzo ya upatanishi yanapaswa kukumbatiwa katika mfumo wa kutafuta haki kwa njia mbadala kwa kuwa kulingana naye mahakama zinaweza kuchunguza na kuamua zile kesi zinazoweza kutatuliwa nje ya mahakama.
Imetayarishwa na Janice Marete