MWAURA: MITANDAO YA KIJAMII INATUMIWA KUPANGA MAPINDUZI AFRIKA

Kufuatia video zinazozungumzia uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore wa Burkina Faso, msemaji wa serikali Isaac Mwaura anasema kuwa watu wenye nguvu wanatumia mitandao ya kijamii kupanga mapinduzi Afrika.
Anasisitiza kuwa kuna operesheni inayohamasisha utawala wa kijeshi, ikiunga mkono mapinduzi na kukosoa viongozi wa kidemokrasia huku akionya kuwa mifumo hii inapaswa kuchukuliwa kwa uzito.
Tangu Traore alipochukua madaraka kupitia mapinduzi dhidi ya Luteni Koloneli Paul Henri Damiba mnamo Septemba 2022, Burkina Faso imeungana na Niger na Mali, kuunda Muungano wa Nchi za Sahel.
Imetayarishwa na Janice Marete