#Rugby #Sports

SENENDE YASHANGAZA NA KUTWAA TAJI LA U19 BLACK ROCK

Timu ya wavulana walio na umri wa chini ya miaka 19 kutoka Shule ya Upili ya Senende iliibuka mabingwa wa wavulana U19 baada ya kuishinda Kakamega High 12-10 katika fainali ya mwisho ya mashindano ya Western Black Rock yaliyofanyika Kakamega.

Mwaka huu mashindano hayo yalihusisha timu 33 katika makundi manne. Kinale Girls waliibuka mabingwa kwa upande wa wasichana kwa kuilaza St. Joseph’s 14-07.

Mkurugenzi Matayo Mwenesi alisifu safari ya miaka 10 ya mashindano hayo, akisema mustakabali uko wazi.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *