OMTATAH MAHAKAMANI KUHUSU WADHIFA WA CAS

Seneta wa Busia Okiya Omtatah na Wakenya wengine watatu wameelekea mahakamni kuishtaki serikali wakitaka kuondolewa kabisa kwa wadhifa wa makatibu waandamizi yaani CAS.
Kwenye kesi hiyo ambapo washtakiwa ni mwaansheria mkuu, tume ya huduma za umma PSC na tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma SRC, walalamishi wanahoji kuwa afisi hiyo sawa na ile ya mkuu wa utumishi wa umma zilibuniwa bila kujali sheria na hivyo zinafaa kuondolewa
Kwa mujibu wa walalamishi, serikali inapanga njama ya kuifanyia sheria marekebisho ili kupata mwanya wa kuanza upya kuwateua makatibu hao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa