#uncategorized

FORD KENYA YAKUHUSU NINI?

Viongozi wa chama cha ford Kenya katika kaunti ya Transnzoia  wamemtaka gavana wa kaunti hiyo  George Natembea kukoma kumshambulia kwa maneno spika wa bunge la kitaifa Moses Masika Wetangula.

Naibu mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Margaret Wanjala amesisitiza kwamba matamshi yake hayatakiyumbisha chama hicho na kwamba wamejipanga ipasavyo katika kivumbi cha uchaguzi wa mwaka ujao.

Kauli sawa imetolewa na wanachama wa ford kenya akiwemo Cleophus Wafula ambaye amegathabishwa na hatua ya viongozi kurushiana cheche za maneno ambayo kulingana naye yanaibua nyufa Zaidi katika jamii ya Mulembe.

Imetayarishwa na: Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *