MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 21 AKAMATWA KUFUATIA MAUAJI YA MUMEWE

Mwanamume mmoja katika kitongoji cha Matuu, Kaunti ya Machakos, ameuawa kwa kuchomwa kisu na mkewe mwenye umri wa miaka 21 katika kile kinaaminika kuwa mzozo wa kinyumbani.
Kulingana na majirani wanaofahamu kisa hicho, mshukiwa alimdunga kisu mumewe baada ya kudai kuwa amekatishwa tamaa naye.
Mwanamume huyo, 23, amedungwa kisu upande wa kushoto wa kifua kulingana na ripoti, na kufariki papo hapo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye anachukuliwa kama mshukiwa wa mauaji, alijichoma kwa kutumia kisu hicho.
Alikuwa akivuja damu na kupelekwa katika hospitali moja eneo hilo ambapo ametibiwa na badae akakamatwa na maafisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Matuu ambako anazuiliwa kwa sasa.
Imetayarishwa na Janice Marete