MOFA WAPANIA KUPATA ALAMA TATU HII WIKENDI

Klabu ya MOFA inalenga kupata alama tatu watakapokutana na Fortune Sacco wikendi ijayo. Kocha wa MOFA, Charles Odero, anasema kuwa baada ya kuishinda Naivas, sasa ni muhimu pia kuwapiku Fortune, kwani analenga kumaliza katika nafasi tatu bora kwenye ligi hiyo msimu utakapotamatika.
MOFA ambao wako katika nafasi ya tano wakiwa na alama 38, alama 14 nyuma ya viongozi wa ligi Nairobi United, watawalika Fortune Sacco siku ya Jumamosi katika Kaunti ya Kisumu.
Imetayarishwa na Nelson Andati