WATU 19 WAKAMATWA KWA KULEWA NA KUTOA FUJO SIAYA

Watu 19 wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha siaya baada ya kukamatwa wakiwa walevi na kusababisha fujo.
Kumi na tisa hao walikamatwa wakati wa msako dhidi ya pombe haramu ulioendeshwa na maafisa wa utawala na wale wa polisi.
Kamanda wa polisi wa siaya Cleti Kimaoyo amesema oparisheni hiyo iliyoongozwa na naibu kamishina Kalekye Kayot ilifanikisha kukamatwa kwa mmiliki wa baa inayouza changaa.
Katika msako huo piki piki 4 zilinaswa na zinazuiliwa katika kituo hicho cha polisi cha siaya.
Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishw mahakamani hii leo.
Imetayarishwa na: Janice Marete.