POLISI RABAI WACHUNGUZA MAUAJI YA DEREVA

Maafisa wa upelelezi eneo la Rabai kaunti ya Kilifi wanachunguza kisa ambapo derewa aliyekuwa akipeleka shilingi elfu 400 katika eneo la ujenzi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Kulingana na polisi George Omondi Pamoja na mkubwa wake ambaye anauguza majeraha walivamiwa na genge la majambazi waliojihami kwa bunduki nje ya benki ya diamond Trust baada ya kuchukua pesa za kuwalipa wafanyikazi.
Kadhalika polisi wanasema kwamba juhudi za kuwatafuta washukiwa hao zinaendelea huku akiwataka wakaazi wa eno hilo kushiriakana na maafisa kuhakikisha kwamba wanadumisha usalama.
Imetayarishwa na: Janice Marete