AFISA MUKHWANA AWAANIKA WAKUU WA POLISI

Imebainika kuwa maagizo ya kumtesa bloga Albert Ojwang kabla ya kifo chake yalitolewa na aliyekuwa naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat kupitia kwa OCS wa kituo cha Central Samson Taalam, aliyemwagiza afisa wa polisi James Mukhwana kuwatumia wafungwa katika kituo hicho kumtesa Ojwang.
Kwenye taarifa ya Mukhwana kwa mamlaka ya IPOA, afisa huyo amekiri kuagizwa na Taalam kutekeleza amri ya Lagat ya kufanya alichokitaja kuwa kumwadhibu Ojwang punde angewasilishwa katika kituo cha Central na maafisa wa idara ya DCI.
Haya yanajiri huku Lagat akijiondoa afisini kwa muda huku waziri wa usalama Kipchumba Murkomen akisema Lagat yuko tayari kupisha uchunguzi.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa