WAKENYA WAPUMUA, KWA MUDA

Serikali imefanyia marekebisho mswaad wa kifedha wa mwaka 2024-25 na kuondoa baadhi ya mapendekezo ya ushuru wa bidhaa muhimu kama mkate na huduma za kutuma pesa kwa njia ya simu kutokana na malalamishi ya wakenya.
Katika taarifa baada ya kikao cha wabunge wa kenya kwanza kilichooongozwa na Rais William Ruto katika Ikulu, mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango katika bunge la kiatifa Kimani Kuria, amesema ushuru wa bidhaa zinazozalishwa humu nchini umetolewa, sawa na kodi ya thamani ya ziada ya bidhaa zinazozalishwa humu nchini.
Hii ina maana kwamba ni bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi pekee ndizo zitakazotozwa ushuru.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa