#Sports

KENYA YAPATA MATOKEO MSETO KATIKA SIKU YA UFUNGUZI YA MICHEZO YA WAVU

Kenya ilikumbana na matokeo mseto katika siku ya ufunguzi wa Mashindano ya Mpira wa Wavu ya Ufukweni ya CAVB Afrika huko Tetouan, Morocco jana Jumatano.

Jairus Kipkosgei na Elphas Makuto walishindwa kwa seti za moja kwa moja 21-18 na 21-13 na Peter Ibrahim wa Nigeria na Uche Augustine katika Ufukwe wa Martil.

Katika mashindano ya wanawake, Gaudencia Makokha na Sharleen Sembel waliondoka na ushindi katika pambano kali dhidi ya wachezaji wawili wawili wa Nigeria, Genevive Kelechi na Happy Wushilang – ushindi ukiamuliwa katika seti ya tatu baada ya timu zote kushinda seti moja kila moja.

Siku iliisha kwa hali mbaya kwa Kenya, hata hivyo, Veronica Adhiambo na Mercy Iminza walilazwa na Nigeria kwa seti 21-18 na 21-8.

Wawili hao awali walikuwa wamewachachafya Nadia Buntubwimana wa Burundi na Emelyne Igiraneza kwa seti moja kwa moja, na kushinda kwa alama sawa za 21-14, 21-14.

Imetayrishwa na Nelson Andati

KENYA YAPATA MATOKEO MSETO KATIKA SIKU YA UFUNGUZI YA MICHEZO YA WAVU

DUKE ABUYA ASHINDA TUZO LA LIGI KUU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *