#Football #Sports

MODO ANA IMANI NA KIKOSI CHAKE

Kocha msaidizi wa Police fc Antony “Modo” Kimani anasalia na matumaini ya kupata matokeo mazuri katika mechi yao ijayo ya marudiano dhidi ya Coffee ya Ethiopia, licha ya kuapata sare tasa katika mchezo wao wa kwanza katika uwanja wa Nyayo juzi jumapili.

Kenya Police FC ilipoteza nafasi ya kutumia vyema faida ya kucheza nyumbani baada ya kulazimishwa sare tasa na wapinzani wao katika mechi yao ya kwanza duru ya mchujo kuwnaia kombe la mashrikisho barani afrika CAF, na Kimani amesisitiza haja ya uchambuzi wa kina ili kujiandaa na mchezo wao wa ugenini.

Kimani pia alisifu kiwango kizuri walicho onyesha lakini akasisitiza umuhimu wa kupiga msasa maeneo kadha ili kujiboresha kwa mechi ya marudiano tarehe 25 mwezi huu.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MODO ANA IMANI NA KIKOSI CHAKE

NANJALA AREJEA NYUMBANI

MODO ANA IMANI NA KIKOSI CHAKE

BADO HATUJAANZA MAZOEZI MUHAMBE ASEMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *