UTATA WA ADANI KUENDELEA, KUNDI LAVURUGA VIKAO KORTINI
Utata kuhusu mpango wa serikali kuukodisha uwanja wa kimataifa wa ndege wa JKIA kwa kampuni ya Adani utachukua muda zaidi kutatuliwa, baada ya mahakama kuu kulazimika kuahirisha vikao vya kusikiliza kesi inayopinga mpango huo.
Jaji wa mahakama hiyo Bahati Mwamuye amelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kundi la watu kuvuruga kikao hicho huku wakiimba nyimbo za kupinga mpango wa kukabidhi usimamizi wa uwanja huo kwa kampuni ya Adani.
Kikao cha leo kimelenga kutoa mwelekeo kuhusu kesi hiyo iliyowasilishwa na mwanahabari Tony Gachoka na wataalamu wa sheria kutoka eneo la Mlima Kenya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































