LIPA HUSTLER FUND AU ‘USALIMIWE’, OPARANYA
Huenda wakenya ambao wamefeli kulipa mkopo wa Hustler Fund wakajipata pabaya baada ya Waziri wa vyama vya ushirika na biashara ndogo ndogo Wycliffe Oparanya kutangaza msako dhidi yao.
Akizungumza jijini Nairobi, Oparanya amesema wizara yake imeanzisha mchakato wa kubuni mfumo utakaofanikisha kuwanasa wakenya hao, na kupongeza hazina hiyo akisema ililenga kubuni nafasi za ajira.
Wakati uo huo, Oparanya amesema serikali itaanza kuwatuza wakenya ambao wamekuwa wakilipa mkopo huo kwa wakati.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































