TULISHAURIANA NA ODINGA KUUNGANISHA NCHI, RUTO

Rais William Ruto amekariri haja ya taifa kuungana na kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali mirengo ya kisiasa, akisema hatua hiyo itasaidia katika kuimarisha utendakazi wa serikali kwa faida ya mwananchi.
Akizungumza kwenye kaunti ya Homa Bay wakati wa ziara yake ya maendeleo, Ruto amesema hatua ya kuwajumuisha viongozi wa upinzani kwenye baraza lake iliafikiwa baada ya mashauriano na kiongozi wa ODM Raila Odinga, huku naibu wake Rigathi Gachaua akikariri haja ya ushirikiano.
Aidha, Ruto ameonyesha matumaini kwamba Odinga atanyakua ushindi wa uongozi wa bara la Afrika, huku gavana wa Homa Bay Gladys Wanga akimpongeza kwa kuwateua viongozi kutoka eneo hilo
Imetayarishwa na Antony Nyongesa