HAKUNA GACHAGUA, HAKUNA SERIKALI: WAKAZI WA NYERI WAANDAMANA KUPINGA HOJA YA KUMTIMUA GACHAGUA

Shughuli za biashara na usafiri katika kaunti ya nyeri zimetatizika pakubwa baada ya wakaazi wa kaunti hiyo kujitokeza kwa wingi kuandamana wakilamikia hoja ya kutimuliwa kwa Gachagua mamlakani
Waandamanaji hao wameziba barabara kuu na kuwasha mioto mikubwa, na hivyo kusababisha shughuli za kila siku kusimama.
Zaidi ya hayo, wakaazi wamedai kuwa baadhi ya maafisa wa serikali walikuwa wakiwapa hongo ya shilingi 500 ili kupata uungwaji mkono wa hoja ya kumtimua Naibu Rais Gachagua.
Imetayarishwa na Janice Marete