MACARTHY ATETEA UTEUZI WAKE WA KIKOSI CHA STARS
Kocha wa Harambee Stars Benni McCarthy ametetea uteuzi wake wa kikosi cha CHAN, mashindano yatakayoanza mwezi ujao.
Raia huyo wa Afrika Kusini anasema alichagua wachezaji bora zaidi wa ndani waliopo, huku kukiwa na mijadala tofauti baada ya kutaja kikosi chake cha kwanza ambacho kiko kambini kwa ajili ya mashindano ya bara.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Tanzania ambapo kitacheza michuano ya mataifa manne ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao.
Wakati huo huo, waziri wa Michezo Salim Mvurya ameahidi kuiunga mkono kikamilifu timu hiyo kuelekea mashindano yao ya CHAN, akisema serikali ina nia ya kuboresha daima miundo msingi ya michezo nchini.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































