Ubao wa Aviation
Katika kijiji cha Luhohwe kilichopo jimbo la Bungoma magharibi mwa Kenya anapatikana mwanaume anayejulikana kama ‘Yesu’ wa Tongareni.
Maisha yake yalikuwa ni ya kawaida hadi ilipofika mwaka 2009 ambapo anadai Mungu alimjia na kumpatia jina Yesu, na kuanzia siku hiyo hapaswi kuitwa au kutaja majina yake ya awali.
Mwandishi wa BBC Roncliff Odit, alipomtembelea hivi karibuni maghribi mwa Kenya, Yesu wa Tongareni alisema aliitwa jina Yesu na Mungu mwenyewe: ”Mungu akanena nami akanipa jina Yesu…
Nawatangazia watu wamrejelee Mungu katika njia ya toba wapate ondoleo la dhambi, ili majina yao yawe katika kitabu cha uzima wa milele” alisisitiza Yesu wa Tongareni kwa sauti ya madaha.
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































