ODM YAPINGA USHIRIKIANO, YADAI KUDHULUMIWA
Chama cha ODM kimeendelea kujitetea dhidi ya madai ya kuwepo kwa mapatano na serikali ya Kenya Kwanza, inavyoenezwa na baadhi ya viongozi wa muungano wa Azimio.
Mwenyekiti wa kitaifa Gladys Wanga ameshikilia msimamo wa kiongozi wa chama hicho Raila Odinga kwamba hakuna mkataba wa ushirikiano na serikali.
Aidha, amesema kwamba viongozi wa ODM walioteuliwa kuwa mawaziri walifanya hivyo kivyao na wala si kwa niaba ya ODM.
Wakai uo huo, Wanga ambaye pia ni gavana wa Homa Bay, amedai kuwa kuna njama ya vyama tanzu katika muungano wa Azimio kuinyang’anya ODM nyadhifa za uongozi bungeni, madai yake yakisisitizwa na naibu kinara wa ODM Godfrey Otsotsi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































