#Football #Sports

HARAMBEE STARS WAJIANDAA KWA MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa Harambee Stars imepata majeraha kwa wachezaji muhimu kabla ya mechi mbili muhimu za kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Malawi mwezi ujao

Engin Firat alisema kuwa mipango yake ya mechi dhidi ya Burundi na Ivory Coast imekuwa ngumu zaidi kwani hadi wachezaji wanane wa kikosi cha kwanza wameathiriwa na majeraha.

Lakini alithibitisha kuwa nahodha na mshambuliaji wa Harambee Stars Michael Olunga, ambaye jina lake halikuonekana katika orodha ya awali ya wachezaji 25 iliyotolewa Jumatatu, atasafiri moja kwa moja hadi Malawi, badala ya kusafiri kupitia Kenya.

Miongoni mwa wachezaji waliojeruhiwa ni mshambuliaji Masoud Juma pamoja na mabeki Dennis Nganga, Eric “Marcelo” Ouma na Joseph Okumu,

Harambee Stars itacheza na Burundi Juni 7 kabla ya kumenyana na Ivory Coast, mabingwa watetezi wa Afrika, siku nne baadaye.

kenya ililazimika kuhamishia mechi zao Malawi baada ya serikali ya Kenya kufunga viwanja vyote vikubwa kwa ajili ya ukarabati, ikimaanisha kuwa hakuna viwanja vilivyoidhinishwa na FIFA.

Kwa sasa Kenya inashika nafasi ya tatu katika Kundi F la kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026, baada ya kuambulia pointi tatu katika mechi zao mbili za ufunguzi dhidi ya Gabon na Ushelisheli. Ivory Coast na Gabon zimefungana mbele kwa pointi sita kila moja kutokana na mechi mbili.

HARAMBEE STARS WAJIANDAA KWA MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

SHUJAA WATUA MIRAMAS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *