MAUAJI YA KWARE: MAHAKAMA YAWAPA POLISI DHAMANA

Mahakama kuu ya Milimani imewapa dhamana ya shilingi 200,000 kila mmoja maafisa wa polisi wanaodaiwa kuwasaidia washukiwa 13 akiwemo mshukiwa wa mauaji ya Kware Collins Khalusia kutoroka kutoka kituo cha Gigiri.
Akitoa uamuzi huo, jaji wa mahakama hiyo Martha Naanzushi amekatalia mbali ombi la polisi kuwazuilia maafisa hao kwa siku 14 ili kukamilisha uchungizi dhidi yao.
Aidha, amewaagiza washtakiwa kuripoti kwa idara ya upelelezi DCI mara mbili kila wiki kwani uchunguzi unaendelea.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa