#Business

UJUMBE WA KINDIKI KWA WAFANYABIASHARA

Naibu Rais Kithure Kindiki amepongeza juhudi za wafanyabiashara katika sekta ya kibinafsi kwa kuoanisha juhudi zao na vipaumbele vya kitaifa, hususan uwezeshaji wa vijana na Agenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi almaarufu bottom-up economy.

Akizungumza wakati wa Maonyesho ya Kazi yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Kindiki amesisitiza dhamira ya serikali ya kuweka mazingira wezeshi kwa biashara za humu nchini na mataifa ya nje huku akizitaka kampuni kutanguliza vipaji vya Wakenya, akibainisha kuwa lengo kuu la serikali ni kuweka nchi kama kitovu cha talanta kinachopendelewa kote Afrika.

Vile vile, kindiki amesema kuwa Teknolojia, vijana, na ushirikiano ni vichochezi muhimu vya uchumi wa siku zijazo, na kuhimiza ushirikiano kati ya serikali, mashirika ya kibinafsi, na taasisi za mafunzo ili kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana na mapungufu ya ujuzi.

Maonyesho hayo ya kazi yalileta pamoja zaidi ya kampuni 60 za Kenya na China, na kutoa nafasi zaidi ya 1,700 za ajira kwa vijana.

Imetayarishwa na Maureen Amwai

UJUMBE WA KINDIKI KWA WAFANYABIASHARA

SHULE ZA KAKAMEGA ZATAMBA MAGHARIBI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *