#Local News

ALIYEKUWA MKUU WA TSC NANCY MACHARIA APATA AJIRA MPYA

Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa tume ya kuwaajiri walimu TSC Nancy Macharia, ameteuliwa na gavana wa Murang’a Irungu Kang’ata kuwa mwenyekiti wa bodi ya huduma za umma kwenye kaunti hiyo, siku chache kabla ya kuondoka kutoka TSC tarehe 30 mwezi huu.

Kupitia kwa waraka kwa bunge la kaunti ya hiyo, Macharia ni miongoni mwa watu wengine 5 walioteuliwa kuhudumu kwenye bodi hiyo, wanachama wakiwa ni Dakta Louis Mwende, Johnson Kang’ethe na Dakta Brian Lishenga, huku Oscar Kimani akiteuliwa kuwa katibu wa bodi hiyo.

Iwapo wataidhinishwa, watahudumu kwa kipindi cha miaka 5, wakiwa na uwezo wa kuongeza mkataba.

Imetayrishwa na Antony Nyonesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *