#Football #Sports

MAN UNITED WAICHARAZA ASENALI 5-3

Wachezaji kumi wa Manchester United waliwalaza Arsenal 5-3 kwa penalti baada ya sare ya 1-1 katika raundi ya tatu ya Kombe la FA. United walilipiza kisasi kufuatia kichapo cha 2-0 kutoka kwa Arsenal kwenye Ligi Kuu mwezi Desemba.

Bruno Fernandes aliwaweka United kifua mbele kwa shuti kali dakika ya 52, lakini Diogo Dalot alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika tisa baadaye. Gabriel Magalhaes aliisawazishia Arsenal dakika ya 63, lakini Arsenal walipoteza penalti muhimu baada ya Altay Bayindir kuokoa mkwaju wa Martin Odegaard.

Kai Havertz alikosa nafasi nyingi, ikiwa ni pamoja na penalti katika mikwaju ya matuta, na Joshua Zirkzee akaipatia United ushindi kwa penalti ya mwisho.

Man United wamegundua tena heshima na imani yao huku Arsenal wakionyesha hitaji lao la kudumu la mshambuliaji wa kati.

Imetayarishwa na Janice Marete

MAN UNITED WAICHARAZA ASENALI 5-3

NAIVAS WAILAZA MSA 4-1 NYUMBANI

MAN UNITED WAICHARAZA ASENALI 5-3

MARY MUTHONI; HAKUNA HMPV KENYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *