MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI KATIKA AJALI YA BARABARANI HUKO NAROK

Mwendesha pikipiki ambaye bado hajatambuliwa amefariki katika ajali ya barabarani iliytotokea usiku wa kuamkia leo katika kaunti ya Narok.
Kulingana na ripoti ya polisi iliyowasilishwa katika kituo cha Polisi cha Narok, ajali hiyo imetokea mwendo wa saa 3:00 asubuhi katika mtaa wa Empopongi, takriban kilomita 8 mashariki mwa Kituo cha Polisi cha Kaunti Ndogo ya Narok ya Kati.
Ajali hiyo imehusisha lori iliyokuwa ikiendeshwa na Hudson Wycliffe Anjere, na pikipiki
Dereva huyo wa pikipiki, anayetajwa kuwa mwanamume Mwafrika mwenye umri wa karibu miaka 30, alikuwa akiendesha upande mwingine wa lori hilo, lililokuwa likitoka Maai Mahiu kuelekea Narok.
Kulingana na ripoti ya polisi, mwendesha pikipiki ameshindwa kuidhibiti na kugongana ana kwa ana na lori hilo na kufariki papo hapo.
Dereva wa lori hajapata majeraha yoyote katika ajali hiyo
Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Narok Level 5 kwa utambuzi na uchunguzi wa baada ya maiti.
Imetayarishwa na Janice Marete