KAUNTI ZADAI NJAMA YA ‘KUPOKONYWA’ AFYA
Baraza la magavana limeibua madai kwamba serikali kuu inapanga njama ya kuirejesha sekta ya afya chini ya usimamizi wa serikali hiyo kupitia tetesi kwamba ugatuzi umeshindwa kuiendesha sekta ya afya.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya afya katika baraza hilo ambaye pia ni gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki, wameilaumu serikali kuu kwa kukosa kutuma shilingi bilioni 100 kwa serikali hizo ambazo ni za mwaka wa kifedha wa 2023-24.
Ameongeza kuwa hadi sasa, serikali hiyo haijatuma mgao kwa miezi mitatu ya hivi punde.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































