IDARA YA MAJANGA YAONYA KUHUSU HALI MBAYA

Mamlaka ya Usimamizi wa majanga nchini NDMA imesema, watu wapatao milioni 1.9 wanahitaji msaada wa chakula, wakati hali ya Uchumi ikizidi kuwa mbaya kati ya mwezi wa Juni na Agosti.
Mamlaka hiyo imetoa ripoti mpya kwa mwezi wa Mei ikisema kuwa idadi kubwa ya waathiriwa wako katika kaunti 23 kame na nusu kame nchini.
Mamlaka hiyo imesema hali inakadiriwa kuwa mbaya zaidi katika mwaka wa kifedha 2024/2025 hasa mwezi June hadi Agosti kwenye baadhi ya kaunti kame isipokuwa sehemu chache.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, utapiamlo mkali umetokea katika kaunti mbalimbali kufuatia hali ngumu ya uchumi, ambako watoto wapatao laki 8.5 wenye umri wa miezi 6 hadi miezi 59 na wajawazito na mama wanaonyonyesha zaidi ya laki 1.2 wanakumbwa na utapiamlo na kuhitaji matibabu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa