MBUNGE OMANYO AITISHA SODO

Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Busia Catherine Omanyo, ameishutumu serikali kwa kuchelewesha pesa za kununua vitambaa vya sodo kwa wanafunzi wa kike, akisema wanahangaika kutokana na ukosefu wa vitambaa hivyo.
Ametoa wito kwa idara husika kurejelea mpango huo kwa manufaa ya wanafunzi wanaohangaika.
Aidha, ametoa wito kwa wahudumu wa boda boda kwenye kaunti hiyo ambao hawajapokea mafunzo ya uendeshaji wa magari kujisajili na kunufaika na mafunzo hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa.