RAILA AENDA KIMATAIFA, SERIKALI KUMZINDUA UGENINI
Juhudi za waziri mkuu wa zamani Raila Odinga kuwania uwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AUC zinatarajiwa kupigwa jeki hii leo kutokana uzinduzi wa azma yake katika jukwa la kimataifa.
Uzinduzi huo umeratibiwa kufanyika alasiri hii katika makao makuu ya umoja wa Afrika AU jijini Addis Ababa Ethiopia, kamati kuu ya kampeni zake ikisema atazinduliwa rasmi na serikali ya Kenya.
Viongozi waalikwa kutoka mataifa uya kigeni tayari wamefika, kujumuika na viongozi kadhaa wa serikali ya Kenya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































