#Sports

MILLAN WAMSAJILI JOAO FELIX

AC Milan imemsajili fowadi wa timu ya taifa ya Ureno Joao Felix kutoka Chelsea kwa mkopo kwa msimu uliosalia, wakati Chelsea wamemleta kiungo Mfaransa Mathis Amougou kutoka Saint-Etienne kwa kandarasi ya miaka minane.

Ripoti za vyombo vya habari vya Uingereza zilisema Amougou, 19, alijiunga na Chelsea kwa ada ya takriban pauni milioni 12 ($14.98 milioni).

Felix alijiunga na Chelsea kutoka Atletico Madrid mwezi Agosti kwa mkataba wa miaka saba kwa ada iliyoripotiwa kuwa ya pauni milioni 46 ($57.16 milioni), lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekuwa na wakati mgumu wa kucheza katika kipindi chake cha pili akiwa na klabu hiyo ya Ligi ya Premia.

Tangu kuwasili kwake Chelsea, Felix ameanza mechi tatu pekee za ligi licha ya kufunga bao kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Wolverhampton Wanderers — bao lake pekee la ligi msimu huu.

Akiwa Milan, Felix atafanya kazi na kocha Mreno Sergio Conceicao.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *